Deni la Trilioni 1.3 aliloacha Micheal Jakson laiweka familia matatani.
Joyce Shedrack
June 29, 2024
Share :
Mshindi wa Grammy mara 13 na mwanamuziki kutoka Marekani Michael Jackson ameacha familia yake kwenye wakati mgumu kwa kuacha deni la dola 500 milioni ikiwa ni sawa na Sh 1.3 Trilioni linalotakiwa kulipwa mapema kutokana na amri ya Mahakama Kuu ya Los Angeles.
Taarifa zinaeleza kuwa wakati msanii huyo anafariki mwaka 2009 aliacha deni litokanalo na ziara yake ya ‘This Is It’ ambapo alikopa pesa ili kufanikisha show hiyo iliyopangwa kuoneshwa zaidi ya mara 50 katika ukumbi wa ‘O2 Arena’ jijini London.
Mahakama Kuu ya Los Ageles imewataka watunzaji wa mali za Micheal Jkson kulipa deni hilo kabla riba haijaongezeka zaidi ya hapo.
Tofauti na deni hilo Michael Jackson pia aliacha deni jingine linalogharimu dola milioni 40 analodiwa na promota wa watalii, AEG.
Michael Jackson alizaliwa August 29, 1958 Nchini Marekani na kufariki June 25, 2009 akiwa na umri wa miaka 50 huku akiacha watoto watatu ambao kwa sasa tayari ni watu wazima mdogo akiwa na umri wa miaka 21.