pmbet

Derby ya Sudan kuchezwa Dar es Salaam

Sisti Herman

June 25, 2024
Share :

Chama cha Mpira wa Miguu nchini Sudan (SFA) kimetuma maombi kwenda Shirikisho la soka Tanzania (TFF) juu ya kuutumia uwanja wa Azam Complex, Chamazi kwa mashindano ya Sudan Super League inayotarajiwa kuanza kurindima kuanzia Juni 25 mpaka Juni 30, 2024.

Taarifa ya TFF imebainisha kuwa mashindano hayo yenye lengo la ujumbe wa kurudisha amani nchini Sudan yatashirikisha timu za Al-Hilal, Al-Merrikh na Al-Wadi Nyala.

Michezo hiyo ya Super League itachezwa kuanzia saa 12 jioni, Ratiba ipo hivi;

- Juni 25, 2024: Al-Hilal SC v Al-Wadi Nyala
- Juni 27, 2024: Al-Wadi Nyala v Al-Merrikh
- Juni 30, 2024: Al-Merrikh SC v Al-Hilal

Picha juu ni wachezaji zamani wa klabu hizo ambao wamewahi kupita Simba SC, Paschal Wawa aliyevaa jezi ya Al Merrikh na Sharaf Eldin Shiboub aliyevaa jezi ya Al Hilal.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet