pmbet

Dhahabu ya shilingi Bilioni 1.5 yanaswa ikitoroshwa

Eric Buyanza

March 20, 2024
Share :

Shehena ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 1.5 imenaswa mkoani Mbeya ikitoroshwa kwenda kuuzwa kusikojulikana, watu 10 wanashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama wakituhumiwa kuhusika na utoroshaji huo.
 

Dhahabu hiyo yenye uzito wa kilogramu 9.8 inadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi Kazi cha Kuzuia utoroshaji madini ikiwa inaandaliwa kusafirishwa na watu hao.
 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema watu hao walinaswa kwenye moja ya nyumba zilizoko katika Mtaa wa Ilomba, jijini Mbeya kufuatia operesheni maalumu iliyofanywa na vyombo hivyo.
 

Amesema shehena hiyo ilikuwa imegawanywa kwenye vipande 334 ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa kwenye vyombo maalum na kwamba watu hao walikutwa na vifaa mbalimbali vilivyokuwa vinatumika kuandalia dhahabu hiyo.
 

Amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni mizani za kisasa za kupima uzito na ubora wa dhahabu, vifaa vya kuchomea dhahabu, mitungi ya gesi, vifaa vya kupoozea dhahabu  na kemikali maalum ya kusafishia dhahabu.
 

“Watu hawa endapo wangefanikiwa kutorosha dhahabu hii, serikali ingepoteza zaidi ya Sh. milioni 144 ambazo ni mrabaha, ada ya ukaguzi, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Ushuru wa Huduma wa Halmashauri,” amesema Mavunde.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet