pmbet

Dhehebu la Orthodox linasherehekea Krismasi leo.

Joyce Shedrack

January 7, 2026
Share :

Leo ni Krismasi kwa Mataifa kadhaa Duniani, yakiadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
 

Mamilioni ya Wakristo wa dhehebu la Orthodox husheherekea Krismasi Januari 7, badala ya Disemba 25, iliyozoeleka na wengi, unaweza kuiita Krismasi ya Orthodox.
In pictures: Orthodox Christians celebrate Christmas - BBC News

Ni sikukuu inayopewa heshima kubwa kwa baadhi ya mataifa hasa ya magharibi.
 

Sababu kuu ya tofauti ya tarehe ya Krismasi iko kwenye matumizi ya kalenda tofauti.
 

Wakristo wa dhehebu la Orthodox hufuata kalenda tofauti na kalenda ya Gregorian ambayo kawaida hutumika katika nchi za Magharibi.
 

Julius Caesar alianzisha kalenda katika 46BC kulingana na ushauri wa mwana-astronomia wa Misri Sosigene, ambaye alikuwa amehesabu mwaka wa mwezi.

 

Lakini vipimo vyake havikuwa sahihi kwa takriban dakika 11, na kwa karne nyingi tarehe za sikukuu za Kikristo zilikuwa zimebadilika sana na ikawa hoja ya mjadala.
 

Ili kurekebisha hili, kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory mwaka wa 1582, na hii ndiyo ambayo mataifa ya Magharibi na maeneo mengi duniani bado yanaitumia hadi leo.
 

Baadhi ya Mataifa yanayosherehekea Krismas ya Orthodos ni Urusi, Bulgaria, Belarus, Egypt, Ethiopia, Eritrea, Georgia, Israel, Kazakhstan, Macedonia, Moldova, Montenegro na Serbia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet