Diamond aandaa bomu jipya..! Ngoma mpya na staa wa Morocco ipo njiani.
Joyce Shedrack
July 31, 2024
Share :
Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz anatarajia kutoa ngoma mpya aliyoshirikiana na msanii kinara wa Morocco mwenye rekodi za kibabe Afrika kwa kuwa na wasikilizaji wengi kwenye digital platforms Saad Lamjarred.
Ukurasa rasmi wa lebo ya WCB Wasafi wa instagram umethibitisha ujio wa ngoma hiyo Kwa kuchapisha picha za wasanii hao wakiwa pamoja Studio na kuandika “Saad Lamjarred & Diamond Coming Soon” .
Saad Lamjarred ni msanii anayesifika kwa kuwa na rekodi bora kwenye Digital Platforms zinapiga muziki huku akitajwa kuwa na wimbo wenye watazamaji zaidi ya bilioni 1.1 huku ngoma zake saba zikiwa na watazamaji Milioni 200 na nyingine 5 zikiwa na zaidi ya watazamaji zaidi Milioni 100 Youtube.
Msanii huyo pia anashikilia rekodi ya kuwa msanii wa pili barani Afrika mwenye Subscribers wengi zaidi akiwa na Subscribers zaidi ya Milioni 15 huku wa namba moja akiwa ni muimbaji wa Misri Mohamed Ramadan Mwenye Milioni 15.6.