Diamond aelekea Zenji kumuomba Zuchu msamaha
Eric Buyanza
February 24, 2024
Share :
Baada ya jana mwanamuziki Zuchu kutokea WCB kutangaza kuwa hayuko tena kwenye mahusiano na Diamond. Leo tarehe 24-Feb Diamond anasema anaelekea Zanzibar kwenda kumuomba Zuchu msamaha.
Haya ndiyo aliyoyaandika;
“Kaka yangu @hajismanara jana alinishauri niache kiburi niende Zanzibar nikaombe Msamaha pengine nitaweza Rudiwa, Baada Kum’bishia kwa Muda Mrefu nikagundua Yuko sahihi…Nami niko njiani kuelekea Zanzibar kuelitekeleza hilo…Nahitaji sana mawazo yenu kwenye Ubunifu wa Kuomba Msamaha”