Diamond afanya balaa Barcelona.
Joyce Shedrack
July 29, 2024
Share :
Staa wa Bongo Fleva Diamond platnumz usiku wa kuamkia leo alifanya show yake ya pili nje ya Afrika huko Barcelona Nchini Uhispania kwenye tukio la Afrobrunch linalojulikana kwa kuadhimisha muziki na tamaduni za Afrobeats.
Diamond alifanya show hiyo akitumbuiza ngoma zake pendwa ikiwemo Komasava inayotambata kwa sasa duniani kote huku umati mkubwa mkubwa wa watu wakionekana kuimba na kucheza ngoma hiyo wakati staa huyo akiwa jukwaani.
Hii inakuwa show ya pili barani Ulaya baada ya siku ya Ijumaa kutumbuiza kwenye show ya Afro Land iliyofanyika Nchini Ujerumani.