Diamond aongoza orodha ya wasanii wenye wafuasi wengi Afrika
Eric Buyanza
March 1, 2024
Share :
Kutoka mitaa ya Tandale mpaka kufika ngazi za juu kabisa kwenye muziki Afrika, ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kwa haraka, hii imejidhirisha baada ya msanii Diamond Platinumz kuwa msanii wa kwanza Afrika kufikisha wafuasi milioni 8.66 kwenye mtandao wa YouTube.
Kwa kufikisha wafuasi hao Diamond ameweza kuwagalagaza kama sio kuwaacha mbali wasanii wakubwa maarufu kutoka Afrika kama Davido, Burna Boy bila kumsahau Wizkid.
Kwenye list hiyo msanii anayemfuatia Diamond, ni Burna Boy (mwenye wafuasi milioni 4.65) anakuja Davido (mwenye wafuasi milioni 3.88) na watatu ni WizKid (mwenye wafuasi milioni 2.99).