pmbet

Diamond ataka Haji afunguliwe kifungo cha TFF

Joyce Shedrack

January 19, 2024
Share :

Msanii wa muziki wa bongo fleva Diamond Platnumz ameuomba uongozi wa Serikali kumfungulia Haji Manara ambaye anatumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa miaka miwili aliyopewa na kamati ya maadili ya TFF mwaka 2022,

Diamond Platnumz amehoji ni kosa gani alilofanya Haji Manara lililofanya kufungiwa kujihusisha na mpira kwa kipindi chote cha miaka miwili

Akizungumzua kwenye Royal Birthday ya Manara & Engagement Party yake na mchumba wake Zaiylissa usiku wa kuamkia leo. Diamond amesema .......

“Mimi nilikua sijui kabisa michezo lakini kupitia Haji nimelijua soka, tufike mahali tuache chuki binafsi, Haji amefanya Kosa gani au dhambi gani kubwa kiasi cha kufungiwa muda wote huo, kila mtu hapa anafahamu Haji ni mtu wa kukata mti na kupanda mti labda ndio sababu kunakuwa na chuki binafsi.

“Viongozi wa Kiserikali mko mahali hapa mnaliona hili labda mtatusaidia Haji afunguliwe,” amesema Diamond.

Ikumbukwe kuwa Julai 2022 Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia  Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili na faini ya Tsh. milioni 20 kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyopigwa Jijini Arusha kati ya Yanga na Coastal Union.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet