pmbet

Diamond na Alikiba jukwaa moja Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma .

Joyce Shedrack

January 16, 2025
Share :

Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya Diamond Platnum na Ali Kiba wanatarajiwa kuwa sehemu ya wasanii watakaotumbuiza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Jijini Dodoma, January 18 na 19, 2025.

Mkutano huo utafanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini humo utashuhudia wasanii hao wakipanda jukwaa moja kwa ajili ya kutumbuiza.

 

Licha ya wasanii hao, lakini kutakuwa na wasanii wengine ambao ni Nandy, Harmonize, Jux, Rayvanny, Zuchu, Marioo na Shilole, Abigail Chams, Mrisho Mpoto, Dulla Makabila, Sholo Mwamba, Samia Queens, Wasoma utenzi Zanzibar, Zanzibar Big Star na Tanzania One Theatre (TOT).

 

Mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

pmbet

pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League

pmbet
pmbet