Diamond na Jasan Derulo wafanya balaa Afrika Kusini.
Joyce Shedrack
September 22, 2024
Share :
Staa wa bongofleva Diamond Platnumz usiku wa jana alijiunga na msanii wa kimataifa wa Marekani Jason Derulo kwenye siku ya kumbukizi ya msanii huyo wa Marekani ya kuzaliwa pamoja na kufanya shoo ya kipekee nchini Afrika Kusini.

Mastaa hao wawili waliambatana na wenyeji wao Chley Nkosi na Khalil Harison ambao walishirikiana kwa pamoja kutumbuiza kwa mara ya kwanza wakitoa burudani kwa mashabiki kupitia wimbo maarufu wa @diamondplatnumz, "Komasava." ambao aliwashirikisha wasanii hao.
Shoo hiyo ilikuwa na msisimko wa kipekee kutokana na wingi wa mashabiki waliohudhuria huku wakifurahia na kushangilia wakati ya perfomance ya ngoma hiyo iliyopendwa Duniani kote.





