Diamond na watoto wake wakimbizana YouTube
Joyce Shedrack
August 13, 2024
Share :
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa rekodi lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz pamoja na wasanii walio chini ya lebo yake wanaendelea kufanya vizuri kwa kuwa wasanii wenye namba kubwa na za kuvutia kupitia digital platform mbali mbali za kuuzia muziki ikiwemo mtandao wa YouTube ambao mpaka sasa yeye pamoja na Msanii wake D Voice ndio vinara On Trending kupitia ngoma walizozitoa hivi karibuni.
Diamond amesimama On Trending namba moja kupitia video remix yake ya Komasava ambayo hivi sasa imefikisha watazamaji milioni 10 baada ya wiki mbili tu toka iachiwe huku msanii wake D Voice akiwa On Trending namba mbili kupitia ngoma yake ya Nani aliyomshirikisha Zuchu iliyotoka Agosti 6 mwaka huu.
Lebo hiyo maarufu ya WCB Wasafi inaundwa na wasanii kama vile Lavalava, Mbosso, D Voice, Zuchu pamoja na Diamond Platnumz mwenyewe.