Diamond Platnumz akanusha Mbosso kutimka WCB.
Joyce Shedrack
February 4, 2025
Share :
Mwanamuziki Diamond Platnumz ametaka watu kupuuza taarifa zozote zinazomuhusu Mbosso kutaka kuondokakwenye lebo ya WCB yeye akiwa kama Muanzilishi na mwenyekiti wa lebo hiyo kubwa ya Muziki Nchini.

Diamond amekanusha taarifa za staa huyo wa bongofleva kujiengua kwenye lebo hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akithibisha wamefanya mazungumzo na Msanii huyo.
"Tumekua na mazungumzo mazuri na Mbosso Namna ya kuanza Rasmi sasa Kusimamia kazi zake na Tumekamilisha jambo letu vizuri sana, Tafadhali story yoyote inayozungumzwa kuhusu jambo hili la Mbosso naomba zipuuzwe, Mpaka mimi binafsi na Mbosso tutakapotoa Tamko rasmi" Diamond Platnumz
Ikumbukwe,Hivi karibuni kuliibuka tetesi za kumhusisha msanii huyo kuondoka chini ya usimamizi wa WCB zilizoanzishwa na mtangazaji maarufu Baba levo.