Diamond Platnumz atangaza Lavalava kujitoa WCB Wasafi.
Joyce Shedrack
May 21, 2025
Share :
Staa wa muziki wa Bongofleva na Mmiliki wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz amethibitisha kumruhusu Msanii wake Lavalava kwenda kujitegemea mwenyewe bila kumlipa gharama zozote.
Diamond amesema hayo siku ya leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Hyatt Regency Hotel alipokuwa akitangaza kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitangaza moja ya kampuni ya vinywaji Tanzania.
“Lavalava ni moja ya wadogo zangu ambao nawapenda sana hakunifata kuniomba kuondoka mimi nilimpigia Kim nikamwambia mwambie Lavalava kama kutoka aje nitampa free release”amesema Diamond.
Aidha,Msanii huyo amesema ikitokea msanii anayetaka kutoka WCB ametozwa fedha basi ni kwa sababi amemkosea adabu na si vinginevyo.
“Ukiona mtu nimemtoza hela ujue kanikosea adabu” Diamond Platnumz.