Diamond Platnumz kushindana na matajiri wakubwa Duniani.
Joyce Shedrack
September 4, 2024
Share :
Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva na mfanyabiashara Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' ameweka wazi kuwa ndoto yake kubwa kwa sasa ni kuwa tajiri namba moja duniani huku akiweka ahadi ya kuwa mtanzania wa kwanza uiweka rekodi hiyo.
Diamond ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye uzinduzi wa Tamasha la Wasafi Festival akweka wazi pia yupo hatua za mwisho kutambulisha biashara zake mbili mpya atakazozifanya kuanzia mwaka huu.
“Ndoto yangu kubwa kwenye maisha ni kuwa tajiri namba moja duniani”
Nyota huyo wa muziki Tanzania kwa sasa anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 10 za Kimarekani sawa na shilingi bilioni 27.1 za Kitanzania anapigania ndoto yake akishindana na matajiri wakubwa Duniani kama Elon Musk, Bernard Arnault, Bill Gates, Aliko Dangote na Jeff Bezos.