Diamondo kuangusha 'show' ya kibabe usiku wa tuzo za CAF 2024
Sisti Herman
December 15, 2024
Share :
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetangaza msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz kuwa mtumbuizaji rasmi kwenye usiku wa tuzo za CAF 2024 utakaofanyika kesho December 16 jijini Marrakech nchini Morocco.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii pamoja na zile za Lebel inayomsimamia, Diamond amethibitisha taarifa hizo.