Diane Rwegara, mkosoaji mkubwa wa Kagame atangaza kugombea Urais
Eric Buyanza
May 9, 2024
Share :
Mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, Diane Rwigara, ametangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X (zamani Twitter), Rwigara amesema anafungua ukurasa mpya kwenye uwanja wa kisiasa na kuwaomba Wanyarwanda wamuunge mkono ili kuweka historia.
Rwigara, mwenye umri wa miaka 42, ni kiongozi wa chama cha People Salvation Movement, alikuwa awanie uchaguzi wa mwaka 2017 lakini hakupitishwa na Tume ya Uchaguzi.
Itakumbukwa mwaka 2017 alipotangaza nia ya kugombea Urais, picha zake za utupu ziliwekwa mitandaoni, katika kile alichodai zililenga kumchafua kisiasa ili kumyamazisha.
Hapo nyuma, aliwahi pia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kughushi nyaraka na uchochezi dhidi ya serikali ya rais Kagame.
VOA