pmbet

Diddy aingia kwenye kesi nyingine ya kunyanyasa wanawake

Eric Buyanza

September 12, 2024
Share :

Rapa maarufu duniani Sean 'Diddy' Combs ambaye kwa miezi ya karibuni amekuwa akiandamwa na kesi nyingi za unyanyasaji nchini Marekani, amefunguliwa kesi nyingine mpya ya unyanyasaji na aliyekuwa mshiriki wa kipindi chake cha 'Making the Band' kilichokuwa kinarushwa na televisheni ya MTV. 

Dawn Richard aliwasilisha malalamiko yake jijini New York dhidi ya Combs na wengine wanaohusishwa naye akidai alishuhudia Rapa huyo akiwatendea vibaya wanawake kwa kuwanyanyasa kimwili na pia aliwahi kushuhudia rapa huyo akimpiga mpenzi wake wa zamani, Cassandra Ventura. 

Wakili wa Combs, Erica Wolff alisema rapa huyo ameshtushwa na madai hayo na kuyaita "ya kutunga na ya uongo".

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet