Diddy amkumbuka "EX" wake
Sisti Herman
December 16, 2023
Share :
Rapa wa kimarekani P. Diddy ambaye anakabiliwa na kesi za unyanyasaji wa kingono, ameuvunja ukimya baada ya kuchapisha kwenye mtandao wake wa Instagram picha ya aliyekuwa mpenzi wake mwanamuziki na model Kim Porter.
Diddy amechapisha picha akiwa na Kim akimtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa huku akiweka wazi kuwa amemkumbuka sana mzazi mwenzie.
Kim Porter na Diddy walikuwa katika mahusiano na walibahatika kupata watoto watatu wawili wakiwa mapacha, Kim alifariki November 15 mwaka 2018 kwa ugonjwa wa nimonia.