Diddy asikitika kushindwa kuhudhuria Graduation ya binti yake
Sisti Herman
June 2, 2024
Share :
Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy juzi alishindwa kuhudhuria kwenye mahafali ya binti yake aitwaye Chance (17) huku wadau wakieleza sababu zilizopelekea kutohudhuria katika sherehe hiyo kufuatia na kesi zinazomkabili.
Mahafali ya Chance Combs yalifanyika katika Shule ya Sierra Canyon huko Los Angeles yalihudhuriwa na familia ya Kim Porter pamoja na mama mzazi wa Chance, Sarah Chapman kama wanavyoonekana kwenye picha ndogo.
Hii imekuwa mara ya pili kwa Diddy kutohudhuria kwenye matukio makubwa ya watoto wake kwani wiki iliyopita alishindwa kuhudhuria kwenye shughuli ya tangazo la biashara ya watoto wake mapacha Jessie na D'Lila.
Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa ngono toka mwishoni mwa mwaka jana, ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana na kesi hizo mahakamani.