Diddy atuhumiwa tena kwa unyanyasaji wa kingono
Sisti Herman
May 23, 2024
Share :
Mwanamitindo Crystal McKinney ametoa shutuma za kunyanyaswa kingono kwa Mwanamuziki na mfanyabiashara Sean Combs “Diddy” ambaye ndani ya miezi michache iliyopita amendamwa na matukio mengi sana yaliyomfanya kutokauka kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali vya habari.
Crystal McKinney akiwa na umri wa miaka 22 anadai alilazimishwa kushiriki ngono ya mdomo bila ridhaa yake akiwa hajitambui.
Mwanamke huyo anasema alikutana na Diddy, Cipriani Downtown NYC Mwaka 2003 katika maonesho ya Mavazi ya Kiume, alipewa mwaliko kumtembelea rapa huyo katika Studio zake anakodai alifanyiwa Ukatili huo
Crystal amedai alimkuta Diddy akiwa na rafiki zake wakitumia Pombe na Kuvuta Vilevi ambapo alilazimishwa Ngono na alipokataa aligongeshwa Kichwa sakafuni kiasi cha kupoteza fahamu na kuja kuzinduka akiwa kwenye gari
Amedai alipata Msongo wa Mawazo na kutaka kujiua mwaka mmoja baadaye, hivyo amefungua Kesi ya kutaka kulipwa fidia ya Udhalilishaji huo.
Ikumbukwe, Novemba 2023, Diddy alifunguliwa kesi pia na aliyekuwa mpenzi wake, Cassie Ventura lakini wakamalizana nje ya Mahakama.