Diddy na Diageo mambo fresh
Sisti Herman
January 17, 2024
Share :
Baada ya kurindima mahakamani kesi iliyofunguliwa na rapa kutoka nchini Marekani P Diddy kwa kuishutumu kampuni ya vinywaji ya Diageo kwa ubaguzi wa rangi, hatimaye rapa huyu na kampuni hiyo wamemaliza tofauti zao.
Kwa mujibu wa jarida la People Diddy na Diageo wamefikia makubaliano ya kumaliza tofauti zao ambapo rapa huyo amefuta mashitaka aliyofungua lakini hawatoweza kuendelea kufanya kazi pamoja kama ilivyokuwa hapo awali.
Ikumbukwe kuwa mwezi Mei mwaka 2023 iliripotiwa kuwa Diddy aliishitaki kampuni ya Diageo kwa ubaguzi wa rangi, baada ya kampuni hiyo kutemana naye huku ikidai kuwa vinywaji alivyokuwa akitangaza ‘rapa’ huyo vilikuwa havifanyi vizuri sokoni kwa sababu alikuwa mtu mweusi.
Diddy amefanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka 15, mara ya kwanza alianza mwaka 2007 akiwa anatangaza bidhaa zao, kufikia mwaka jana walitemana na ndipo Diddy akafungua kesi dhidi ya kampuni hiyo.