Dieng wa Al Ahly kucheza Valencia mwezi June
Sisti Herman
February 24, 2026
Share :

Klabu ya Valencia CF imekamilisha usajili wa kiungo wa Mali, Aliou Dieng, ambaye atajiunga na timu hiyo mwezi Juni kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Al Ahly SC kumalizika.
Baada ya kuongeza beki wa kati Justin De Haas, klabu hiyo ya jiji la Valencia imefikia makubaliano ya mdomo na Dieng, mwenye umri wa miaka 28, ambaye atatua rasmi pindi mkataba wake wa sasa utakapomalizika.
Inaelezwa kuwa kiungo huyo tayari amefaulu vipimo vya afya, baada ya daktari wa Valencia kusafiri hadi Misri kwa ajili ya kuthibitisha utimamu wake wa mwili. Ingawa klabu haitatoa taarifa rasmi hadi mkataba uanze kutumika, makubaliano kati ya pande zote yamekamilika kwa asilimia mia moja.
Dieng, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Mali, anatambulika kwa nguvu zake za mwili, uwezo mkubwa wa kurejesha mipira, pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya kimkakati. Akiwa na zaidi ya mechi 250 katika soka la Misri, amejiimarisha kama mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Al ahly
Valencia ilijaribu kumsajili mapema katika dirisha la Januari, lakini sasa ataongeza nguvu katika safu ya kiungo kuelekea msimu ujao.





