pmbet

Dili la Bilioni 71 layeyuka baada ya Gabriel Jesus kugoma kwenda Napoli

Eric Buyanza

August 20, 2026
Share :

Gabriel Jesus wa Arsenal hana mpango wa kuhamia Napoli licha ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil, mwenye umri wa miaka 29.
 

Mwandishi wa habari za usajili, Matteo Moretto ameripoti kuwa mchezahi huyo amekataa ofa ya Napoli kwakuwa bado ana hamu ya kucheza Uingereza, huku klabu za Everton na Ipswich zikionyesha nia ya kumsajili.

 

Kutokana na msimamo huo wa Jesus, Napoli chini ya kocha Massimiliano Allegri sasa imeanza kuangalia washambuliaji wengine mbadala kama Joshua Zirkzee wa Manchester United na Nicolas Jackson wa Chelsea.

 

Kama sio ugumu wa mchezaji huyo kugoma kuondoka Uingereza, Arsenal walikuwa tayari kumuuza kwa kiasi cha pauni milioni 20 (sawa na bilioni 71.5 za kitanzania).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet