pmbet

Dili la Dani Olmo kumrithi De Bruyne limekufa rasmi

Sisti Herman

July 26, 2024
Share :

Dili la kiungo mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzg Dani Olmo kujiunga na Manchester City kurithi nafasi ya kiungi mshambuliaji 'mwandamizi' wa klabu hiyo Kelvin De Bruyne ambaye anataka kuondoka hivi karibuni linadaiwa kutoweza kutokea tena dirisha hili licha ya kuwa kwenye hatua nzuri baada ya klabu ya Barcelona kuingilia kati na kutoa ofa nzuri iliyoshawishi upande wa mchezaji na timu yake ya sasa.

Barcelona imekubali kulipia ada ya uhamisho ya Euro Milioni 60 (zaidi ya Tsh Bilioni 176) kwaajili ya kumnasa Dani Olmo kama klabu yake ilivyohitaji ili kusajiliwa Barca, ambapo mgawanyiko wa fedha hizo utakuwa;

- Euro milioni 40 (zaidi ya Tsh Bilioni 117) italipwa kwa awamu kila ifikapo mwezi Januari kuanzia mwaka 2025,

- Euro Milioni 10 (zaidi ya Tsh bilioni 29) italipwa kwa kigezo cha kushinda mataji mawili ya La Liga misimu 5 ijayo,

- Euro milioni 10 zingine ni kwa kigezo Cha kushinda UEFA mbili katika misimu 5 ijayo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet