“Dk Janabi kanifanya ninywe chai isiyo na sukari” – Ummy Mwalimu
Eric Buyanza
January 11, 2024
Share :
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza jana Januari 10, 2024 kwenye mkutano wake na vyombo habari jijini Dar es Salaam kuongelea mafanikio katika sekta ya Afya....aliwafurahisha waandishi baada ya kugusia kidogo kuhusu mafundisho ya Dk Janabi ambayo baadhi yake yamekuwa gumzo kwenye mitando ya kijamii.
"Watu wanafanya mzaha na Profesa Janabi na mafundisho anayotoa japo wakati mwingine hata mimi ananitisha, mimi ni mwanafunzi wake na ameniharibu tangu Mei mwaka jana sinywi chai yenye sukari," alisema Waziri Ummy