pmbet

Dk. Mpango, asema yuko tayari kujiuzulu mradi usipokamilika

Eric Buyanza

March 22, 2024
Share :

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, amesema yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake, endapo mradi mkubwa wa Maji wa Mwanga/Same/Korogwe unaotarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi 438,000 hautakamilika kufikia Juni, mwaka huu. 

Mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300, unafadhiliwa na serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa na mashirika ya misaada ya kimataifa kutoka nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu.

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo jana alipotembelea na kukagua mradi huo katika kijiji cha Kiria, Mwanga mkoani Kilimanjaro.
"Sina uso wa kuja kuwatazama wananchi hawa walioahidiwa upatikanaji wa maji kwa miaka 19 iliyopita. Mimi nitajiuzulu ila sijui nini kitatokea kwa walioko chini yangu, hasa Waziri wa Maji na waliko chini yake.

“Viongozi wa wizara, mradi huu uwe eneo lenu la kudumu. Hakikisheni maji haya yanapatikana. Ikiwa kuna changamoto zitatueni kabla. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (Nurdin Babu) kwa kusaidiana na walioko chini yako, pangeni ziara za kutosha hapa;  nami nitakuja  kabla ya muda huo hapa," amesema. 

Katika maelekezo yake, Dk. Mpango amemkumbusha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri, wakati wa kiapo chake kushika wadhifa huo, Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa maelekezo kwa wizara  hiyo kwamba ifikapo Juni, mwaka huu, maji yapatikane Same na Mwanga (Kilimanjaro) na Korogwe (Tanga).

"Nafikiri ulisikia ‘very clear’ (kwa ufasaha). Jana nilikuwa naongea na Waziri wa Maji (Jumaa Aweso); nataka nirudie tena mjipange vizuri. Wasimamieni makandarasi, bahati nzuri mmesema hapa wana uwezo, usiku na mchana maji yatoke mwezi Juni.

“Mradi huu umekuwa  kero kwa wananchi wa maeneo haya. Wewe hesabu kuanzia 2014 wakati umeanza kutekelezwa. Pangeni zamu za kuja hapa usiku na mchana. Wekeni kempu (kambi) hapa," amesisitiza.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet