Dkt. Mpango awasili Uswizi kumwakilisha Samia WEF
Sisti Herman
January 14, 2024
Share :
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, leo January 14, 2024 amewasili nchini Uswisi ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) utakaofanyika tarehe 15 hadi 19 January 2024 katika mji wa Davos.
Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya uchumi na uwekezaji, utawala bora, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kilimo na pia atafanya mazungumzo ya uwili na Viongozi wa Mataifa na Mashirika mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.