pmbet

Dkt. Mwinyi Amteua Arafat wa Yanga kuwa Mkurugenzi PBZ

Sisti Herman

May 9, 2024
Share :

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua makamu wa rais wa Yanga Sc, Arafat Ally Haji kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ). Kabla ya uteuzi Ndugu Arafat alikuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC).

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwinyi amemteua Balozi Omar Yussuf Mzee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA). Mhe. Balozi Omar ni Mstaafu katika Utumishi wa Umma.

Rais Mwinyi amemteua Dkt. Huda Ahmed Yussuf kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Aidha Dkt. Mwinyi amemteua Ndugu Saleh Saad Mohamed kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA). Kabla ya uteuzi Ndugu Saleh alikuwa Msaidizi Mkurugenzi Huduma za Uwekezaji ZIPA.

Wakati huo huo aliyekuwa Mkuu wa Divisheni ya Mipango, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Dkt. Haji Gora Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kitaifa na Uratibu wa Diaspora katika Ofisi ya Rais Ikulu.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet