Dkt. Tulia aongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano wa IPU
Sisti Herman
February 13, 2025
Share :
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson ameongoza Kikao cha Kamati ya Maandalizi cha Mkutano wa 6 wa Maspika Duniani, unaotarajiwa kufanyika Julai 2025 mjini Geneva, Uswisi.
Mkutano huo umefanyika Februari 12, 2025 katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa (UN), uliopo jijini New York, Marekani huku ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Viongozi hao ni pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa IPU, Maspika, Manaibu Spika na Wakuu wa Misafara wa Mabunge ya China, Uingereza, Nigeria, Hispania, Bahamas, Malta, Azerbaijan, Ivory Coast, Mexico, Uswisi, Algeria, Malawi, Canada na Qatar.