pmbet

Dodoma yawavuta pamoja Ajibu, Lusajo na Waziri Jr

Sisti Herman

July 26, 2024
Share :

Baada ya kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa zama ni wa Yanga na Simba Ibrahim Ajibu kutokea Coastal Union klabu ya Dodoma Jiji imeendelea kujiimarisha kwa kuwanasa washambuliaji bora wawili kwenye ligi kuu wa miaka kadhaa sasa Reliant Lusajo na Waziri Junior.

Dodoma wamemnasa Waziri Junior kutokea KMC ambapo alikuwa mfungaji bora wa pili kwa wachezaji wazawa baada ya Feisal Salu kwenye msimu wa ligi uliomalizika.

Dodoma wamemnasa Lusajo kutokea Mashujaa aliyojiunga nayo msimu uliopita akitokea Namungo.

Wachezaji hao wazoefu wa Ligi Kuu wanaenda kukutana na ni wazi kama watakuwa kwenye ubora wao basi safu ya Ushambuliaji ya Dodoma itatisha sana msimu ujao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet