pmbet

Dogo afaidi game ya dezo kutoka kwenye dirisha la chumba chake!

Eric Buyanza

October 28, 2026
Share :

Picha ya kijana mdogo aliyekuwa anatazama soka bila kulipa kiingilio imekuwa gumzo mtandaoni. Kijana huyo alionekana akishuhudia mubashara timu ya Fleetwood Town ikiwabandua mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Arsenal, bila kulipa hata senti moja.

 

Tunaweza kusema alipata "VIP seat" ya kipekee moja kwa moja kutoka kwenye dirisha la chumba chake cha kulala kinachotazama ndani ya uwanja wa Highbury Stadium unaomilikiwa na Fleetwood Town.

 

Kutoka dirishani kwake, alishuhudia Fleetwood Town inayoshiriki Ligi Daraja la Nne (League Two) ikiandika historia ya kuitoa Arsenal kwa mikwaju ya penati 5-3, kufuatia sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida.

 

Mchezo huo wa raundi ya nne pia uligubikwa na matukio ya kushangaza ikiwemo mchezo kusimamishwa kwa dakika nane baada ya droni isiyojulikana kupaa uwanjani, pamoja na kinda wa miaka 16 wa Arsenal, Max Dowman, kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Kipa wa Fleetwood, Jay Lynch, alikuwa shujaa kwa kupangua penati ya Bruno Guimarães kabla ya Conor Haughey kupiga penati ya ushindi iliyoipeleka Fleetwood robo fainali kwa mara ya kwanza kihistoria.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet