pmbet

Dogo Ahmed atengeneza saa, polisi wamtia pingu wakidhani ni bomu

Eric Buyanza

July 6, 2026
Share :

Kijana mmarekani mwenye asili ya Sudan, Ahmed Mohamed ambaye alijipatia umaarufu mkubwa duniani mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 14, baada ya saa ya kidijitali aliyoitengeneza nyumbani kudhaniwa kuwa ni bomu na uongozi wa shule yake huko Texas, Marekani.

 

Ahmed alikuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza na alikuwa akipenda sana masuala ya sayansi na uhandisi. Siku moja alichukua 'circuit board' na skrini ya kidijitali, akaviunganisha ndani ya kisanduku kidogo ili kutengeneza saa ya kengele.

 

Baada ya utundu huo kukamilika, aliibeba saa hiyo na kwenda nayo shule kwa nia njema ya kumwonyesha mwalimu wake wa masomo ya uhandisi ili kuonyesha kipaji chake. Mwalimu huyo alimwambia kuwa saa hiyo ilikuwa nzuri, lakini akamshauri asiwaonyeshe walimu wengine.

 

Wakati wa somo la Kiingereza, saa hiyo ililia ikiwa ndani ya mkoba wake. Ahmed alimwonyesha mwalimu huyo wa Kiingereza, lakini mwalimu alishtuka na kusema kifaa hicho kinafanana na bomu.

 

Uongozi wa shule uliita polisi. Ahmed alikamatwa akafungwa pingu mbele ya wanafunzi wenzake, na kupelekwa kituo cha kulelea watoto watukutu (juvenile detention center).

 

Polisi walimhoji kwa saa moja na nusu bila wazazi wake kuwepo. Ahmed alisisitiza kuwa ni saa tu, na mwisho wa siku polisi walibaini kuwa kifaa hicho hakikuwa na hatari yoyote na hawakumfungulia mashtaka yoyote ya jinai.

 

Picha ya Ahmed akiwa amevaa fulana ya NASA huku akiwa amefungwa pingu ilisambaa kwa kasi sana kwenye mitandao ya kijamii. Wengi walikasirishwa na kitendo hicho wakiamini amewekewa wasifu wa kigaidi kwa sababu tu ya  asili yake.

 

Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg alimwalika Ahmed kutembelea makao makuu ya Facebook na kumpongeza kwa ubunifu huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet