pmbet

Dogo aishi peke yake miaka 2 baada ya mama yake kukimbilia kwa bwana!

Eric Buyanza

January 27, 2024
Share :

Magazeti ya Ufaransa hivi majuzi yameripoti kisa cha kushtua na kuhuzunisha kilichoumiza wengi ambapo dogo (mvulana) wa miaka 9 alilazimika kuishi peke yake katika nyumba yenye baridi kali kwa miaka miwili mfululizo baada ya mama yake mzazi kuhamia kwa Bwana (mpenzi).
 

Inaelezwa kuwa kati ya mwaka 2020 na 2022 mvulana huyo ambaye jina lake halikutajwa aliishi kwa kula pipi, chakula cha makopo na kutegemea hisani kutoka kwa majirani huku mama yake akiishi kwa raha katika nyumba ya mpenzi wake umbali wa kilomita 5 tu kwenye mji uitwao Sireuil.
 

Mama yake alikuwa akimtembelea mara moja moja sana lakini hakukaa kwa muda mrefu na hakuwahi kumpeleka kwenye nyumba anapoishi na mpenzi.
 

Taarifa zinasema majirani walichoshwa na hali hiyo na kuamua kuwashirikisha polisi.
 

Tangu mvulana huyo alipowekwa katika uangalizi maalum kwenye sehemu za kulelea watoto, mama yake aitwae (Alexandra) alienda kumtembelea mara mbili tu na baadae kukata mawasiliano naye.
 

Jambo la kushangaza ni kwamba, licha ya hali yake ya kusikitisha, mvulana huyo alienda shuleni kila siku na kufanya vyema darasani ...kiasi kwamba walimu wake hawakuwahi kushuku lolote.
 

Mama yake alifunguliwa mashataka na tayari amehukumiwa kwenda jela miezi 18 kwa kutelekeza mtoto.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet