pmbet

Dogo amuua mpenzi wa mama yake baada ya kuwafumania jikoni

Eric Buyanza

May 30, 2024
Share :

Huko Kericho nchini Kenya katika Kijiji cha Ririat, limetokea tukio lililoshtua wengi ni baada ya mvulana mwenye umri wa miaka 16 anayesoma kidato cha kwanza kwenye Shule ya Sekondari ya Kabarus Day, kumuua mpenzi wa mama yake kwa kumchoma na kisu.
 

Aliyechomwa kisu ni Michael Rono mwenye umri wa miaka 65, na imeelezwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa, mvulana huyo alikasirishwa baada ya kuwakuta mzee huyo na mama yake wakifanya mapenzi jikoni.
 

Mercy Mutai, jirani aliyesikia ugomvi uliohusisha watatu hao, anasema alimsikia mvulana huyo akizozana na marehemu Michael Rono (mpenzi wa mama) na kuanza kumpiga kabla ya kuamua kuchukua kisu na kumchoma mara mbili kifuani.

Mtu huyo alikufa papo hapo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet