Dogo aogelea masaa 4 baharini kwenda kuikoa familia yake
Eric Buyanza
April 20, 2026
Share :
#JeWajua January 30,2026 huko nchini Australia dogo wa miaka 13 aliyetambulika kwa jina la Austin Appelbee aligeuka shujaa baada ya kuogelea kwa takriban masaa 4 (karibu kilometa 4) kwenye maji yenye mawimbi makali ili kumuokoa mama yake pamoja na wadogo zake wawili waliosombwa na maji.
Wakati haya yanatokea yeye na familia yake walikuwa likizoni wakivinjari katika eneo la watalii la pwani kusini mwa mji wa Perth.
Hata hivyo Austin anasema hajawahi kujiona shujaa kwa kitendo alichokifanya kwa kuwa alifanya kile alichopaswa kukifanya.






