Dogo avumbua kifaa kitakachowawezesha vipofu kutembea bila fimbo
Eric Buyanza
July 8, 2024
Share :
Kutana na Khalifa Aminu, ambaye amevumbua aina ya miwani yenye 'sensor' itakayowasaidia vipofu kutembea bila kutumia fimbo.
Khalifa ambaye ni mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka 17, anayeishi Kano nchini Nigeria, anasema amefanya uvumbuzi huo ili kuwasaidia vipofu duniani kote na anaendelea tafiti za kukiboresha kifaa hicho.