Dogo wa miaka 17, ashtakiwa kwa mauaji ya mabinti watatu nchini Uingereza
Eric Buyanza
August 1, 2024
Share :
Mtoto wa miaka 17 ameshtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu katika hafla ya kucheza densi huko Southport.
Bebe King, 6, Elsie Dot Stancombe, 7, na Alice Dasilva Aguiar mwenye umri wa miaka tisa walifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kisu kwenye hafla iliyopewa jina Taylor Swift katika mji wa Merseyside siku ya Jumatatu.
Kijana huyo, ambaye anatazamiwa kufikishwa katika mahakama ya jiji la Liverpool baadaye Alhamisi, pia ameshtakiwa kwa makosa 10 ya kujaribu kuua.
Watoto wengine wanane na watu wazima wawili waliokuwa kwenye hafla hiyo walijeruhiwa, huku baadhi yao wakiaminika kuwa bado katika hali mbaya.
Mshitakiwa ambaye jina lake halikuweza kutajwa kwa sababu ya umri wake pia amefunguliwa shtaka la kumiliki kifaa butu.
Polisi wa Merseyside walitangaza mashtaka hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.