Doku kurejea kambini baada ya kuhudhuria kuzaliwa kwa mwanae.
Joyce Shedrack
June 23, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Ubelgiji Jeremy Doku amerejea kambini mwa timu ya taifa siku ya leo baada ya kuondoka kwa muda na kusafiri kwenda London Uingereza kuhudhuria kuzaliwa kwa mwanawe.
Doku alikosolewa vikali sana na mwandishi wa habari pamoja na wanasoka kwa uamuzi wake wa kuondoka kambini ili kuwa pamoja na mke wake, kukutana na mwanawe mchanga, na kushuhudia moja ya nyakati muhimu zaidi maishani mwake
Hata hivyo Jeremy alienda London, akatimiza wajibu wake kwa familia, kisha akarudi kambini na hata hatakosa mechi yoyote ya Kombe la Dunia kwani sasa anapatikana tena kwa kikosi cha Ubelgiji.





