Don Carlo alivyobadili Midfield ya Brazil kimajukumu ndani ya mechi 2
Sisti Herman
June 23, 2026
Share :

Utangulizi
Katika mechi mbili za mwanzo za Kombe la Dunia 2026, dhidi ya timu za taifa za Morocco na Haiti, timu ya Taifa ya Brazil imeonyesha sura mbili tofauti kabisa katika eneo la kiungo kimuundo na kimajukumu ambapo kwenye mchezo dhidi ya Haiti, kocha mkuu wa timu hiyo Carlo Ancelotti alionekana kuyafanyia kazi mapungufu yaliwafanya kupata sare kwenye mchezo wa kwanza wa kundi L dhidi ya Morocco.
Utofauti wa Muundo wa Midfield
Dhidi ya Morocco
Dhidi ya Morocco, Brazil ilicheza zaidi katika muundo wa 4-3-3 ambao mara nyingi uligeuka kuwa 4-1-4-1 wakati wa kujilinda. Casemiro alikuwa kiungo wa chini (single pivot) mbele ya mabeki. Bruno Guimarães na Lucas Paquetá walicheza kama namba 8 wawili wenye majukumu ya kusaidia mashambulizi lakini pia kurudi chini kulinda maeneo ya pembeni ya Casemiro.

Lengo kuu la mfumo huu lilikuwa kuzuia transitions za haraka za Morocco kupitia maeneo ya kati. Morocco ilitumia sana kasi ya wachezaji wake wa pembeni, hivyo Brazil ilihitaji kuwa compact katikati ya uwanja. Katika mfumo huu, viungo watatu walikuwa karibu sana ili kupunguza nafasi kati ya mistari ya timu.
Dhidi ya Haiti
Dhidi ya Haiti, Brazil ilicheza kwa muundo uliokuwa wa kushambulia zaidi. Mara nyingi mfumo ulionekana kama 4-1-3-2 au 4-4-2 Diamond wakati wa kumiliki mpira. Casemiro alibaki chini kama namba 6 huku Bruno Guimarães na Paquetá wakisogea juu zaidi. Matheus Cunha alikuwa akishuka kutoka mstari wa ushambuliaji kuingia katikati ya uwanja na kuunda superiority ya idadi dhidi ya viungo wa Haiti.

Hii ilisababisha Brazil kuwa na wachezaji wanne katikati ya uwanja, yaani Casemiro, Bruno Guimarães, Paquetá, Cunha tofauti na dhidi ya Morocco. Kutokana na hali hiyo.
Mapungufu ya Kimbinu dhidi ya Morocco
Dhidi ya Morocco Changamoto kubwa waliyopitia, Brazil ilipitia changamoto kubwa ya kimuundo kudhibiti mashambulizi ya kujibu (Negative Transitions) hasa nyakati ambazo Paqueta na Guimarez wakisogea juu kuunganisha washambuliaji wa pembeni na mabeki wao ili kuweza kupenya kuta za Morocco, kisha timu ikipoteza mpira na kujibiwa shambulizi kwa haraka kabla hawajarejea kwenye umbo lao mama la kuzuia.

Casemiro alilazimika kuzuia eneo kubwa mbele ya mabeki wake kwani umbo la Brazil kwenye mistari miwili ya nyuma (Rest Defence) lilikuwa na wachezaji watatu tu, Marquinhos, Gabriel na Casemiro juu yao huku na kwasababu Paqueta na Guimarez walikuwa mbele zaidi kukawa na nafasi kubwa iliyomvuta Casemiro mbele zaidi ya mabeki wake wawili.

Ubora wa Kimbinu dhidi ya Haiti
Dhidi ya Haiti Brazil mabadiliko ya kimuundo yalionekana kuwa na faida wazi ambapo iliweza kutawala mchezo, kiuzuiaji na kiushambuliaji, ikibadili muundo kutoka ile 4-3-3 dhidi ya Morocco na kuwa 4-1-3-2 (4-4-2 diamond) ambapo alipunguza idadi ya washambuliaji na kuwabakiza wawili huku Matheus Cunha akicheza kama kiungo mshambuliaji, tofauti na mwanzo ambapo Igor Thiago alicheza kama mshambuliaji wa kati.

Hii iliwasaidia kudhibiti mchezo kwa kuwa na mpira nyakati nyingi, kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na hata nyakati mpira ukiwa kwa Haiti waliweza kuurejesha haraka kwenye umiliki wao kwasababu ya idadi kubwa ya viungo waliokuwa nao.
Majukumu ya viungo dhidi ya Haiti
Casemiro
Casemiro alikuwa kiungo wa chini (single pivot). Kwenye muundo alisimama mbele ya mabeki, majukumu yake timu ikiwa na umiliki wa mpira yalikuwa kushiriki kuendeleza mashambulizi yanayojengwa kuanzia nyuma kwa mabeki wake kwa njia ya kati (Central Build up Progressions) pia kusimama mbele ya mabeki kuzuia mabeki wake kufikika kirahisi mashambulizi ya kujibu pale timu yake inapopoteza mpira m,bele (Negative Transitions).

Timu yake isipokuwa na mpira nyakati zote alisimama mbele ya mabeki wake kuzuia kufikika kirahisi na kupora mipira mingi na hata aliweza kuwa-Cover pindi wanapotoka kwenye maeneo yao huku takwimu za FIFA zilionyesha alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokimbia umbali mkubwa zaidi katika mchezo huo.

Bruno na Paquetá
Dhidi ya Haiti, Bruno alikuwa kiungo wa kuunganisha safu. Alishuka karibu na Casemiro wakati wa build-up lakini pia alipanda mbele kusaidia presha na kutengeneza nafasi. Ushawishi wake katika kurejesha mipira na kuanzisha mashambulizi ulionekana wazi kwenye mabao ya Brazil.

Dhidi ya Haiti, Paquetá alicheza upande wa kushoto wa kiungo cha watu watatu na mara nyingi alikuwa akijiunga na Vinicius Jr na Cunha kutengeneza triangles za mashambulizi. Alikuwa na uhuru mkubwa wa kuingia kwenye half-space ya kushoto na kusaidia katika final third, ushirikiano wake na Cunha uliipa Brazil uwiano bora zaidi kuliko mechi ya kwanza.

Pasi ya kwenye picha ya juu aliyopiga kwenda kwa Vini Jr nyuma ya ukuta wa Haiti ilienda kuzaa goli la Matheus Cunha ambaye alifunga kwa kushinda Second Ball.

Matheus Cunha
Dhidi ya Haiti, Cunha alikuwa tofauti kabisa na mshambuliaji wa kawaida. Alishuka katikati kusaidia viungo, aliongoza presha ya juu na mara nyingi aliingia kwenye maeneo ya kati ili kuvuta mabeki nje ya nafasi. Mfumo huu ulimsaidia kufunga mabao mawili na kuipa Brazil fluidity kubwa zaidi katika mashambulizi.

Hitimisho
Dhidi ya Morocco, Brazil ilicheza midfield yenye mwelekeo wa kudhibiti hatari za mpinzani na kulinda transitions. Casemiro, Bruno Guimarães na Paquetá walikuwa na majukumu ya uwiano kati ya ulinzi na ushambuliaji.
Dhidi ya Haiti, Brazil ilicheza midfield ya kushambulia zaidi ambapo Matheus Cunha aliongezwa kama kiungo wa nne wakati wa kumiliki mpira. Mfumo huo uliifanya Brazil kutawala katikati ya uwanja, kutengeneza overloads nyingi na kucheza kwa uhuru mkubwa zaidi wa kushambulia.





