Donnarumma atambulishwa rasmi Man City.
Joyce Shedrack
September 2, 2025
Share :
Klabu ya Manchester City imemtambulisha rasmi golikipa wa Timu ya Taifa ya Italia Gianluigi Donnarumma kuwa mchezaji wao akitokea PSG kwa mkataba wa miaka mitano hadi mwaka 2030.
Donnarumma anajiunga na Man City kuchukua nafasi ya Ederson aliyekuwa golikipa namba moja wa timu hiyo ambaye anajiunga na Fenerbahce ya Uturuki.