Dortmund waitoa PSG UEFA, Wawatangulia Madrid na Bayern Wembley
Sisti Herman
May 8, 2024
Share :
Baada ya kushinda kwa jumla ya mabao 2-0, numbani na ugenini, klabu ya Borrusia Dortmund imefanikiwa kufuzu hatua ya Fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo itachezwa kwenye dimba la Wembley jijini London Uingereza mwishoni mwa mwezi huu.
Dortmund watasubiri kumjua mpinzani wao leo usiku kwenye nusu fainali nyingine kati ya Real Madrdi na Bayern Munich.
Goli la pekee la Dortmund jana lilifungwa na beki mkongwe wa klabu hiyo Mats Hummels dakika ya 50 ya mchezo.