pmbet

DR Congo hatarini kutokushiriki Kombe la Dunia 2026 kisa Ebola.

Joyce Shedrack

May 23, 2026
Share :

Kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo kilichoitwa kwa ajili ya Kombe la Dunia kitawekwa karantini kwa siku 21 kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani kutokana na mlipuko wa Ebola kwenye Nchi yao la sivyo kitajiweka mashakani kushiriki Kombe la Dunia.

Nigeria left to blame 'voodoo' after dramatic playoff defeat by DR Congo |  World Cup 2026 qualifiers | The Guardian

DR Congo kwa sasa imepanga kufanya mazoezi nchini Ubeljiji baada ya kambi yao ya mazoezi iliyokuwa ifanyike mjini Kinshasa kufutwa.

 

Andrew Giuliani, mkurugenzi mtendaji wa Kikosi Kazi cha Ikulu ya Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia, alisema kikosi hicho lazima kibaki ndani ya Karantini maalumu nchini Ubeljiji.

 

“Wanahitaji kudumisha hiyo karantini vinginevyo wanaweza kushindwa kusafiri kwenda Marekani. Hatuwezi kuwa wazi zaidi ya hapo,” 

 

“Ikiwa watakuja na yeyote kati yao akaonyesha dalili za ugonjwa, basi wanaweka hatarini timu nzima kushindwa kuja na kushiriki katika Kombe hili la Dunia.”

 

Marekani imepiga marufuku kuingia kwa watu wasiokuwa raia wa Marekani ambao wamekuwa DR Congo, Uganda au South Sudan ndani ya siku 21 zilizopita.

 

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet