Dr Dre apewa Nyota Hollywood Walk of Fame
Sisti Herman
March 20, 2024
Share :
Baada ya kutangazwa na watoaji wa nyota za heshima ya Hollywood Walk of Fame siku chache zilizopita, hatimaye rapa na mtayarishaji wa muziki Dr Dre tayari ametunukiwa nyota hiyo siku ya jana Machi 19.
Dr Dre ametunukiwa nyota hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika muziki pamoja na kuinua wanamuziki mbalimbali akiwemo 50 Cent, kupitia lebo yake.
Katika tukio hilo mastaa mbalimbali walijitokeza kumsindikiza mwanamuziki huyo kwenda kupokea nyota yake ya heshima akiwemo Snoop Dogg, 50 Cent, Eminem na wengineo.