Drake msanii wa kwanza kwenye historia kufikisha 'streams' Bilioni 100
Eric Buyanza
June 19, 2024
Share :
Rapa wa Canada, Drake, anakuwa msanii wa kwanza katika historia kufikisha 'Streams' Bilioni 100 kwenye Spotify.
Mwanamuziki huyo ana zaidi ya mara mbili ya 'streams' za rapa Eminem ambaye ndiye anayemfuatia.
Wimbo wake uliotiririshwa zaidi ni wa mwaka wa 2016 uitwao ‘One Dance’ aliomshirikisha Wizkid, ambao wenyewe tu peke yake una streams Bilioni 3.2.
Wimbo 'One Dance’ unashikilia Rekodi ya Dunia ya Guinness ya kuwa wimbo wa kwanza kuzidi streams Bilioni 1 kwenye Spotify.