Drake ni mkali mara milioni ya Kendrick Lamar – Kanye West
Eric Buyanza
April 3, 2025
Share :
Rapa mtata wa Marekani Kanye West ameibuka na kusema Drake ni mkali mara milioni ya Kendrick Lamar. Kanye alisema haya kwenye mahojiano ya hivi karibuni na DJ Akademiks.
"Jambo moja ni kwamba, Drake ni bora mara milioni kuliko Kendrick Lamar na muhimu mara milioni kwa ulimwengu wa hip-hop.” akasisitiza Kanye.
Maoni ya Kanye West yamezua mjadala mkubwa ndani ya jamii ya hip-hop, haswa ukizingatia kuwa Kendrick Lamar ni rapa anayekubalika sana kwenye kizazi cha sasa.