Drogba alikuwa na tabia za kike - Obi Mikel
Eric Buyanza
January 23, 2024
Share :
Kiungo wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel amesema mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya Chelsea, Didier Drogba alikuwa ana tabia kama za kike za kupenda kusifiwa-sifiwa wakati walipokuwa pamoja Stamford Bridge.
Nahodha huyo wa zamani wa Super Eagles alisema kuwa kipindi hicho Drogba alikuwa anataka kupangwa kwenye mechi kubwa tu na ni mtu kupenda kusifiwa.
Drogba alikuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani wakati wa kipindi chake na alifunga mabao 104 na kutengeneza assist 64 wakati alipokuwa Chelsea.
“Drogba anapenda michezo mikubwa na anaifurahia,” Obi Mikel alisema kwenye Podcast yake ya ObiOne.
"Tulipokuwa na michezo midogo, kama vile Kombe la FA au kucheza dhidi ya vilabu vidogo kama Stoke au vilabu vingine vidogo, hakuwahi kutaka kucheza michezo hiyo hata kidogo."
"Kwake, ilikuwa michezo mikubwa kama Ligi ya Mabingwa au dhidi ya Manchester United na Liverpool, ndipo unapomuona Didier Drogba."
"Didier ana tabia za kike....ukimsifia-sifia (ukimjaza) atafanya vizuri. Lakini siku zote alikuwepo kwa ajili yetu katika mechi kubwa,” aliongeza.