Droni ya Wahouthi yazuiwa kupiga Makka
Sisti Herman
September 16, 2026
Share :

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Saudi Arabia vimesema nchi hiyo imezuiwa droni ya Wahouthi karibu na Makka.
Vikosi hivyo vya ulinzi wa anga vya Saudi Arabia vimesema viliizuia na kuiharibu droni hiyo iliyokuwa imerushwa na waasi wa Wahouthi kutoka Yemen.
Kwa mujibu wa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vya Yemen, tukio hilo limetokea wakati wa ongezeko la mashambulizi ya makombora na droni yanayolenga maeneo mbalimbali.
Msemaji wa muungano huo, Turki al-Maliki, amesema hii ni mara ya pili kwa Wahouthi kujaribu kulenga Makka.
Amesema jaribio la kwanza lilitokea Julai 2017, wakati kombora la masafa marefu lilirushwa kuelekea eneo hilo.
Wakati huohuo, tahadhari ya kiusalama ilitolewa kwa muda mfupi Jumanne, Septemba 15, katika miji ya Makka, Jeddah na Taif.
Hata hivyo, mamlaka za ulinzi baadaye zilitangaza kuwa hali ilikuwa salama na kwamba "hatari imetoweka".
Tahadhari iliyotolewa mjini Makka imevuta umakini kutokana na kwamba mji huo haujawahi kushuhudiwa tukio la aina hiyo katika kipindi cha hivi karibuni.
Siku moja kabla, mashambulizi ya makombora na droni yaliyotekelezwa na Wahouthi dhidi ya miji mitatu nchini Saudi Arabia yaliwajeruhi raia 13, kwa mujibu wa muungano huo.
Muungano huo pia ulisema nyumba saba na magari mawili yaliharibiwa katika mashambulizi hayo.
Chanzo BBC News





