Dube aaga rasmi Azam
Sisti Herman
March 7, 2024
Share :
Mshambuliaji Prince Dube raia wa Zimbabwe ametangaza kuachana na Azam FC baada ya kudumu klabuni hapo kwa miaka minne
Hivi karibuni zilitoka taarifa za mshambuliaji hiyo kuomba kuondoka ,Azam FC walithibitisha taarifa hizo na kuweka wazi kuwa hawamzuii ila taratibu za kuvunja mkataba zifuatwe.
Jana kwenye mechi dhidi ya Coastal Union [FT 1-1] Dube hakuwa sehemu ya kikosi na leo asubuhi ametangaza kuondoka Klabuni hapo.