Dube aomba kuondoka, Azam waweka ngumu
Sisti Herman
March 5, 2024
Share :
Klabu ya Azam FC imethibitisha kupokea barua kutoka kwa mshambuliaji Prince Dube akiomba kuvunja mkataba wa kuwatumikia Waoka Mikate hao ambao amewatumikia tangu mwaka 2020.
Mkataba wa nyota huyo raia wa Zimbabwe aliosaini mwaka 2023 utamuweka klabuni hapo mpaka 2026. Hivyo sasa amebakisha miaka miwili na nusu mkataba wake kufikia ukomo.
Azam FC imemjibu Dube (27) kwamba kama anataka kuondoka kama ambavyo amewasilisha ombi lake, klabu haina kipingamizi chochote na imemruhusu kuondoka lakini matakwa ya mkataba yanatakiwa kutekelezwa ikiwemo kulipa dola za kimarekani 300,000/-.